Dokta Cheni Aeleza Mazingira ya Kifo cha Mdogo Wake Aliyefariki Kwa Ajali – Video

Global Publishers
April 14, 2026
0 Comments

Msanii wa filamu na mshereheshaji maarufu wa Bongo, MC Dr Cheni, ameeleza kwa masikitiko makubwa mazingira ya kifo cha mdogo wake, Mansoor Awadh, aliyefariki dunia kufuatia ajali ya gari.

Akizungumza na vyombo vya habari, MC Dr Cheni amesema alipokea taarifa za ajali hiyo akiwa nje ya nchi, ambapo inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Manyoni wakati marehemu akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Rukwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ajali hiyo ilisababisha kifo cha papo hapo cha Mansoor Awadh, tukio ambalo limeacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.

Aidha, taarifa zinaeleza kuwa mazishi ya marehemu yalifanyika jana katika makaburi ya Kisutu Cemetery jijini Dar es Salaam, ambapo ndugu na waombolezaji walijitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa marehemu.

Tukio hilo linaendelea kuombolezwa na jamii ya wasanii na wadau wa burudani nchini, huku MC Dr Cheni akiendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa watu mbalimbali.