KAMPUNI ya Meridianbet imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya dhati ya kurejesha kwa jamii kupitia zoezi lake endelevu la kusaidia familia zenye changamoto, hususan wajane, katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Katika mwendelezo wa juhudi hizi, Meridianbet ilitembelea eneo la Kijitonyama Kisiwani, ambapo ilikutana na familia kadhaa zinazokabiliwa na changamoto za maisha, na kutoa msaada wa mahitaji muhimu ya kila siku ikiwemo chakula na mahitaji mengine ya msingi.
Vilevile, Michezo mingi zaidi ya kubashiri inaendelea kupatikana ndani ya Meridianbet ikiwa na ODDS kubwa na machaguo mengi zaidi. Kushiriki ni vyepesi kupitia tovuti ya MERIDIANBET au kwa kupiga *149*10#.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet alieleza kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa mafanikio yake yanapaswa kwenda sambamba na ustawi wa jamii inayoiunga mkono. Alisisitiza kuwa kusaidia wajane ni sehemu ya dhamira ya kampuni katika kuhakikisha kuwa kundi hilo linapata faraja na matumaini mapya ya maisha.
“Tunatambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika jamii licha ya changamoto wanazopitia. Meridianbet itaendelea kusimama nao bega kwa bega,” alisema.
Wananchi wa eneo hilo walipokea msaada huo kwa furaha kubwa, wakieleza shukrani zao kwa Meridianbet kwa kuwajali na kuwafikiria katika kipindi kigumu wanachopitia.
Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi ya kijamii (CSR), ikilenga kugusa maisha ya Watanzania na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.