Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, ameeleza kwa kina dhana ya ubia (PPP) akisisitiza kuwa si ubinafsishaji, bali ni mfumo wa ushirikiano unaolenga kuongeza ufanisi na tija katika miradi ya maendeleo ya umma.
Akizungumza na wadau wa sekta binafsi jijini Dar es Salaam, Kafulila alisema mkanganyiko uliopo miongoni mwa wananchi unatokana na kufananisha PPP na ubinafsishaji, huku akifafanua kuwa katika ubia, Serikali hubaki na umiliki wa rasilimali zake huku sekta binafsi ikishiriki katika uwekezaji na uendeshaji.
Alieleza kuwa kuanzishwa kwa sera ya PPP mwaka 2009 na sheria ya mwaka 2010 kulilenga kurekebisha changamoto za mikataba ya nyuma, na kuhakikisha kuwa pande zote Serikali na wawekezaji—zinanufaika kwa usawa na kwa uwazi.
Kwa mujibu wa Kafulila, sababu kuu tatu zinazoifanya Serikali kuingia ubia ni pamoja na kutumia mtaji wa sekta binafsi badala ya kutegemea kodi za wananchi pekee, kupata teknolojia ya kisasa, na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa miradi.
Aidha, alitofautisha kati ya mkandarasi wa kawaida na mwekezaji wa PPP, akieleza kuwa mkandarasi hulipwa baada ya kukamilisha kazi, wakati mwekezaji wa PPP huwekeza fedha zake na kurejesha gharama kupitia uendeshaji wa mradi kwa muda maalum.
Picha za Pamoja.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
