…..
Na. Sixmund Begashe, Njombe
Club ya Michezo ya Maliasili na Utalii (MNRT SPORTS CLUB) imetinga kambini na kuendelea na mazoezi mazito tayari kwa kukabiliana na Club zingine za Michezo katika michuano ya Michezo ya Mei Mosi 2026 Mkoani Njombe.
Baadhi ya Wakazi wa Njombe walioshuhudia mazoezi ya Club wameonesha kuvutiwa kujituma kwenye mazoezi hayo chini ya Mwalimu nguli Bw. Gabriel Mazika, huku wapenzi wa Club hiyo yenye wachezaji mahiri na machachari wakiwa na matarajio makubwa ya ushindi wa kishindo.





