********
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amefanya ziara katika eneo la makumbusho ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere yaliyopo Mwitongo, Butiama mkoani Mara na kuwataka watanzania kumuenzi Kiongozi huyo kwa kuendelea kulipa Kodi kwa hiari.
Akizungumza wakati wa ziara yake Aprili 14, 2026 ikiwa ni siku moja baada ya siku ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Kamishna Mkuu Mwenda amesema enzi za uhai wake Mwl. Nyerere alikuwa akihimiza sana ulioaji wa kodi ili kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi.
Amesema lengo la ziara yake Butiama ni kwenda kushukuru kwa misingi ambayo Mwl. Nyerere aliiweka katika masuala ya kodi kwa kuhimiza kila mtanzania aliyetakiwa kulipa kodi analipa na kodi hiyo inakusanywa kwa uadilifu na kurudi kwa watanzania kwa kupitia miradi ya maendeleo ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema msingi uliowekwa na Baba wa Taifa umeendelea kuenziwa hadi hivi sasa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusimamia ukusanyaji wa kodi kwa kutoa miongozo kwa TRA ili kuiwezesha Tanzania kujitegemea kwa kikasi kikubwa kiuchumi.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuwakaribu na Walipakodi, kuwasikiliza, kutatua changamoto zao, kuwezesha biashara zao.
Katika ziara hiyo Kamishna Mkuu Mwenda ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa ikiwa ni sehemu ya kumuenzi





