DAR YAENDELEA KUNG’ARA MBIO ZA MWENGE UHURU 2026

⅘ (6) Wilaya ya Kigamboni yapitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi hata mmoja uliokataliwa.

Mwenge wa Uhuru 2026 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa huo ambapo Wilaya ya Kigamboni miradi 6 yenye thamani 19,425,732,411.80 imepitiwa na Mwenge hakuna mradi uliokataliwa

Aidha katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru 2026 umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama, Mradi wa kikundi cha vijana Suluhu na Mipango kinachojishughulisha na usafilishaji wa abilia, Ujenzi wa barabara ya Lingia- Nyakwale kwa kiwango cha lami na zege km 3.7, mradi wa usambazaji maji kigamboni loti III, ujenzi wa nyumba ya watumishi kituo cha afya Tundwi Songani, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, matundu 10 ya vyoo na kichomea taka shule ya Sekondari kibugumo, na ujenzi wa Hospitali ya Qualitas Kigamboni.

Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 15, 2026 unaendelea Wilaya Temeke ambapo utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Tanzania ni Yetu Sote,Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo

Mwenge wa Uhuru Oyeeeee…….