Global Publishers
April 15, 2026
0 Comments
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania kuanzia wahitimu wa kidato cha nne hadi vyuo vikuu.
Taarifa ya JWTZ iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano, Luteni Kanali Kevin Byabato, imeeleza kuwa vijana wenye sifa zilizoainishwa, watume maombi kwenda makao makuu ya jeshi hilo, Msalato mkoani Dodoma kuanzia leo Jumatano Aprili 15 hadi Aprili 28, 2026.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
