KITUO TGCL NA KAS CHAANDAA MIJADALA YA UJUMUISHWAJI AFRIKA MASHARIKI

*******

Kituo cha Tanzania na Ujerumani cha Mafunzo ya Sheria za Afrika Mashariki (TGCL) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Konrad Adenauer Stiftung (KAS) Tanzania, kimeandaa mfululizo wa mijadala wa mwaka mmoja kuhusu Mradi wa Ujumuishaji wa Kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika enzi ya Akili Mnemba (AI).

Mdahalo utafanyika mwezi Juni 2026. Wadau wote wenye wanakaribishwa kushiriki.