Global Publishers
April 21, 2026
0 Comments
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa taarifa ya mafanikio ya operesheni maalum iliyofanyika mwezi Aprili 2026, ikihusisha kukamata dawa za kulevya pamoja na pombe haramu aina ya Moshi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo pia imefanikisha ushughulikiaji wa kesi mbalimbali mahakamani, hatua inayotajwa kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu na kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mbali na mafanikio hayo, Jeshi hilo limeeleza kuwa linawashikilia watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio la mauaji ya Emmanuel Pascal yaliyotokea Aprili 20, 2026 katika kata ya Olasiti jijini humo.
Polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo na mazingira ya mauaji hayo, huku wakiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
