Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya mkutano na wadau wa mazingira tarehe 15 Aprili 2026 katika ukumbi wa Maji House, ndani ya jengo la MWAUWASA jijini Mwanza.
Lengo la mkutano ni kukumbusha wadau kuhusu haki na wajibu wao katika kuzingatia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.
Katika mkutano huo, wawekezaji walisisitizwa kuhakikisha wanafanya usajili na kukamilisha mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (ESIA) kabla ya kuanza miradi yao.
Aidha, wataalamu washauri wa mazingira walikumbushwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa kutoa taarifa sahihi na kuepuka udanganyifu.
Kwa upande mwingine, taasisi za serikali zikiwemo halmashauri zilihimizwa kuimarisha ushirikiano katika kusimamia Sheria za mazingira.
Taasisi za Serikali zilizoshiriki ni pamoja na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Halmashaur za wilaya za Mwanza, Bonde la Ziwa Victoria, TBS, jeshi la polisi la zima moto, OSHA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, TMDA









