Serengeti Premium Apple Yazinduliwa Kihistoria Ndani ya Serengeti National Park

Global Publishers
April 20, 2026
0 Comments

Serengeti Premium Apple imeandika historia kwa kuwasilisha uzinduzi wa kipekee ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ikiweka alama kama kinywaji premium (RTD) cha kwanza kutengenezwa Tanzania na kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL).

Kupitia matukio ya uzinduzi kwa siku tatu mfululizo, zaidi ya mastaa na watengeneza maudhui 30 kutoka sekta mbalimbali za ubunifu walisafirishwa kwa ndege binafsi kutoka Dar es Salaam mpaka Serengeti, wakipata fursa ya kushiriki na kufurahia matukio ya kipekee yaliyounganisha na ladha laini na ya kuburudisha ya kinywaji hicho, utamaduni na mandhari ya asili ya Tanzania.

Safari hiyo ilijumuisha matukio mbalimbali yaliyopangiliwa kwa ustadi na ubunifu, kuanzia mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, safari ya ndege binafsi angani, mpaka mapokezi ya kipekee ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Mastaa hao walipata nafasi ya kushiriki shughuli kama vile kutembelea na kujionea mbuga, chakula cha mchana (brunch) na cha jioni (dinner) katika mazingira ya kuvutia kilichoambatana na tafrija fupi. Siku iliyofuatia walishiriki kwa pamoja tukio la kipekee la “Toast in the Sky” lililofanyika kupitia ‘hot air balloon’ juu ya anga la Serengeti. Wageni waalikwa waliandaliwa shughuli tofauti zinazoonyesha namna kinywaji hiki kipya kinavyoweza kuakisi ubora na maisha ya kisasa yenye hadhi ya kimataifa.

Uzinduzi huu uliakisi kwa vitendo misingi mikuu ya chapa mpya ya Serengeti Premium Apple, ikiwemo ladha laini na ya kuburudisha ya apple; fahari ya bidhaa ya Kitanzania inayowakilisha ubunifu, usasa na mafanikio ya Mtanzania wa kisasa; pamoja na kuhamasisha Watanzanie kuendele kuvumbua na kufurahia uzuri na maeneo mapya nchini, ladha mpya na mtazamo mpya wa maisha.

Kupitia uzinduzi huu, kampuni ya Serengeti Breweries Limited imeonyesha uwezo wa Tanzania kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango vya kimataifa huku ikitumia utajiri wa rasilimali zilizopo kama jukwaa la kuonesha ubunifu na hadhi ya juu.