Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Charles Hirali Msangi (34) kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyosababisha abiria 57 kunusurika kifo katika eneo la Mikumi, kando ya barabara kuu ya Mikumi–Ifakara.
Ajali hiyo ilitokea Aprili 16, 2026, ambapo basi lenye namba za usajili T 289 EAG lililokuwa likiendeshwa na mtuhumiwa huyo liliacha njia na kupinduka kutokana na mwendo wa hatari.
Basi hilo lilikuwa likitoka Ifakara kuelekea Dar es Salaam likiwa na jumla ya abiria 57.
Kutokana na ajali hiyo, abiria 13 walijeruhiwa na kupatiwa matibabu katika vituo vya afya vilivyo karibu.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.
Imeandaliwa na Farida Mangube.