BUSHIRI YAIFUNGA MASAIKA, AWESO VIJANA CUP

………………..

NA – MWANDISHI WETU, PANGANI

Mashindano ya Aweso Vijana Cup yameendelea kwa kasi ambapo Aprili 16, 2026, yalizikutanisha timu kutoka Kata ya Bushiri na Masaika ambapo Bushiri ilipata ushindi wa (1-0), mechi iliyochezwa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Masaika.

Katika mechi hiyo, Timu ya Bushiri ilipata goli lake la ushindi kupitia kwa mchezaji wake, Rashid Taube, dakika ya 15 ya mchezo.

Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera amesema mashindano hayo yameongezeka hamasa ya vijana kupenda michezo.

“Mwamko ni mkubwa, vijana wa Pangani wanajitokeza sana katika mashindano haya, na yamesaidia sana kupunguza idadi ya vijana kujiingizia katika makundi mabaya, sasa michezo imekuwa sehemu muhimu ya maisha yao,” amesema Kibendera.

Mashindano ya Aweso Vijana Cup yanahusisha timu kutoka Kata zote 14 za wilaya ya Pangani, chini ya udhamini wa Mbunge wa Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.