VIJANA ZAIDI YA 700 DAR WATAKIWA KUJENGA UWEZO

*******

Na. Mwandishi Wetu, Dar.

MAADHIMISHO ya miaka 20 ya Siku ya Matendo Mema (Good Deeds Day) Nchini yamefanyika  Aprili 18, 2026 Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Don Bosco, Oysterbay, Tukio hilo limewakutanisha vijana zaidi ya 700 na taasisi 40 kwa ajili ya Elimu, burudani, na kujifunza namna ya kubadili matendo mema kuwa mifumo endelevu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, alisisitiza kuwa kipimo cha mtu sio cheo au pesa, bali Uwezo.

“Uwezo wa kufikiri, kudhibiti hisia, na kujijenga ndio unaojenga mustakabali. Sio wengi wanaotenda mema, inahitaji ujasiri, muhimu ni kujenga uwezo,” amesema Murtaza.

Ameongeza kuwa, Uwezo wa msingi huanza utotoni na huwajenga vijana kuendelea kuchangia jamii bila kukata tamaa.

Kwa upande wake,Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa, amesema mwaka huu harakati zinaongozwa na kauli mbiu “Tuungane pamoja katika kufanya matendo mema kutoka moyoni”. Lengo ni kuhimiza watu kutenda mema kwa hiari, kwa kutumia muda, ujuzi na maarifa waliyonavyo.

“Tunasisitiza fikiri wema. Ukifikiria mema, utazungumza mema na hatimaye utatenda mema. Dunia inaweza kuwa salama zaidi endapo kila mmoja atachukua jukumu,” amesema Doroth.

Good Deeds Day huadhimishwa kila Aprili na inachangia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kupitia uhifadhi wa mazingira, afya, elimu, usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini.

Baadhi ya wadau na taasisi na mashrika ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali yaliyoshiriki ni pamoja:UTT AMIS, Dar City promotions,Coca Cola.

Wengine: Natalia Foundation, Rotaract, Mega We Care, PGN Career Solutions, Young life Tanzania, Mental Health Africa, Builders of Future, ⁠Sana Mare. One Health Society, Ingu group, Jenga Wellness Hub,  ⁠Fahari Tuamke Maendeleo, Afya Connect Digital Doctors, Lupus Tanzania Organisation, ⁠Youth Voice Organization na wengineo.