Rais Donald Trump wa Marekani, kwa upande mmoja, analimezea mate eneo lote la ardhi ya Canada ambalo ni mwanachama wa NATO, na kwa upande mwingine, ameonyesha kuwa, ana dhamira ya kuinyakua sehemu kubwa ya ardhi ya Denmark, ambayo nayo pia ni mwanachama wa shirika hilo la kijeshi.
Hasira za Trump dhidi ya shirika kuu la kijeshi la nchi za Magharibi zinazidi kushtadi siku baada ya siku. Katika siku za karibuni, rais huyo wa Marekani aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social: “NATO haikutusaidia huko nyuma na wala haitatusaidia katika siku za usoni.”
Maelezo hayo ya Trump yanaashiria msimamo wa shirika la jeshi la NATO wa kukataa kujiunga na Washington katika vita vya kichokozi ilivyoanzisha kwa mamlaka na Israel dhidi ya Iran. Wakati wa mashambulio ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yaliyoanza tarehe 28 mwaka huu kwa muda wa takriban siku 40, wanachama wa NATO zilikataa kujiingiza katika vita hivyo. Baadhi ya viongozi wa wanachama wa NATO walitamka kinagaubaga kuwa vita hivyo na vita vinavyohusu NATO na hakuna sababu ya kuishambulia jeshi la Iran.
Kwa mujibu wa mkataba wa NATO, endapo nchi moja wa shirika itashambuliwa, nchi zingine wanachama wote zitakuwa na wajibu wa kujiunga na vita ili kumhami mwanachama mwenzao, ukiwa na msingi wa kujihami kwa pamoja. Kwa kuzingatia kuwa Iran haikuwa imeishambulia kijeshi mnamo Februari 28, kanuni ya kujihami kwa pamoja haikupata msingi wa kisheria wa kutumiwa na wanachama wa NATO. Muelekeo huo uliofuatwa na shirika la kijeshi la Magharibi umemhamakisha na kumkasirisha sana Marekani, ambaye nchi yake ndiye mwanachama mkuu. Katika wiki za hivi karibuni, Trump amerudia mara kadhaa matamshi makali ya kejeli dhidi ya NATO na nchi wanachama wake ikiwa ni pamoja na kuliita shirika hilo la kijeshi la Magharibi ‘chui wa’ karatasi.
Lakini mbali na hayo, Trump amewahi mara moja kutamka hadharani kwamba anafikiria kuiondoa Marekani katika NATO, hatua ambayo kama itachukuliwa, itapelekea kusambaratika taasisi hiyo kuu ya kiusalama ya nchi za Magharibi. Hii ni pamoja na kuwa, la Marekani tayari limeshapitisha sheria inayosisitiza kujiondoa Marekani katika NATO kutawezekana kutangazwa kwa idhini ya hilo, na haionekani kama bunge huo ulio na Trump utaweza kupata uungaji mkono wa Kongresi.
Pamoja na hayo, inavyoonekana, Trump anakusudia vita vyake vya maneno dhidi ya NATO pamoja na vitisho vya kujiondoa katika shirika hilo laonekana, huku akiendelea kuzibana nchi wanachama zikubali kutekeleza ratiba ya kushupalia vita inayofuatiliwa na Marekani katika kila pembe ya dunia, kuanzia Ukraine na Venezuela hadi Iran na China.
Wakati huohuo, mielekeo ya rais wa sasa wa Marekani kutumia mabavu na vitisho dhidi ya NATO imezua hofu na wasiwasi mkubwa miongoni mwa mbili wa kijeshi wa Marekani katika pande za Atlantiki.
Bila kujali maoni ya wanachama wengine wa NATO kuhusu vita vya Ukraine, Trump ameishinikiza Kiev ikubali kutoa sehemu ya ardhi ya nchi hiyo kwa ajili ya kumaliza vita na Urusi; hatua ambayo imewatia hofu washirika wa Marekani wa barani Ulaya.
Lakini na hayo, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, utawala wa sasa wa Marekani unaoongozwa na Donald Trump, umekuwa ukiingilia masuala ya ndani ya wanachama wa NATO kwa namna inayolenga vyama vyama vya kihafidhina na wanasiasa hao wanaomshabikia Trump wanaingia madarakani.
Katika anga kama hiyotanda hofu na shaka kubwa ya wanachama wa NATO kwa Marekani ya Trump, rais huyo wa Marekani anaendelea kulalama na kuhoji, kwa nini taasisi hiyo ya kijeshi iliyoiunga mkono sera za Washington. Hii ni katika hali hatima ya kuridhia matakwa ya Trump ni kuishia kukanyagwa maslahi ya kitaifa ya nchi ambazo wanachama wa NATO na kuzifanya nyenzo tu za kutumiwa na rais huyo mbinafsi wa Marekani. Kuonyesha ungangari wa kupinga matakwa hayo kumemkasirisha sana Trump na kuhatarisha umoja na mshikamano wa ndani ya shirika hilo la kijeshi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa…/