YANGA inapiga kotekote. Imempiga nyingi Mbeya City kule kwenye Ligi Kuu Bara, yakazuka maneno kwamba ushindi huo una walakini, ikatua hapa Zanzibar nako kuna timu ya Muembe Makumbi City ika-pigwa nne, sasa baada ya mchezo huo kocha wa mabingwa hao, Pedro Goncalves akafunguka.
Akizungumza jana, Pedro alisema ushindi ambao Yanga wanaupata hautokani na nguvu nyingine zaidi ya ubora wa kikosi chake uwanjani na kuzitaka timu nyingine kuheshimu hilo.
Pedro alisema kila ambapo Yanga inashinda husikia maneno mengi yasiyo na heshima kuhusu kikosi chake, lakini ikishinda taarifa hizo zinabadilika na kugeuzwa kivingine.
Kocha huyo raia wa Ureno alisema watu wa soka wanatakiwa kuifuatilia Yanga kwa kuiheshimu na ub-ora wake, ambapo ndio timu ambayo inaongoza msimamo wa ligi ikiwa haijapoteza na imeruhusu mabao machache.
“Huwa tukishinda tu nasikia watu wanaongea vibaya kuhusu timu yetu, sidhani kama hii ni sawa, watu wanatakiwa kutuheshimu, tunaposhinda ni suala la ubora wetu na ndio maana tunaongoza ligi kule na hapa tumekwenda nusu fainali,” alisema Pedro.
“Kuna wakati tunapata shida kutokana na changamoto zetu na tumekubali, lakini kuna wakati tunaku-tana na magumu ambayo yako nje ya utaratibu, tumeendelea kupambana wenyewe kama timu kubwa, hakuna lingine, kuihusisha Yanga na mambo ya kukosea heshima hiyo siyo sawasawa, nadhani tunastahili kupewa heshima yetu.”
Vilevile Pedro aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri dhidi ya Muembe Makumbi akisema kila eneo lilifanya vyema na timu nzima iliupiga kama bingwa ambaye anatamani kulinda heshima yake.
“Unaona jana (juzi) tulibadilisha kikosi kwa kiwango kikubwa lakini bado unaweza kuona idara ya ulinzi ilifanya vizuri kwenye kuzuia, lakini eneo la kiungo nalo lilifanya kazi kwa uimara na kule mbele tuka-tumia nafasi za kufunga,” alisema kocha huyo.
“Naiheshimu sana Muembe Makumbi, lakini kama tungetumia nafasi kwa wingi zaidi tungeweza kushinda kwa kiwango kikubwa kuliko haya mabao manne. Nadhani tutaendelea kuonyesha ubora mkubwa.” Yanga ilitangulia kutinga nusu fainali ya Muungano ambapo sasa inasubiri kujua itakutana na nani kati ya KVZ iliyokuwa inakutana na Azam FC jana usiku kwenye mchezo wa robo fain