MNRT SPORTS CLUB YAJIFUA, NJOMBE

…..

Na. Sixmund Begashe, Njombe

Club ya Michezo ya Maliasili na Utalii (MNRT SPORTS CLUB) imetinga kambini na kuendelea na mazoezi mazito tayari kwa kukabiliana na Club zingine za Michezo katika michuano ya Michezo ya  Mei Mosi 2026 Mkoani Njombe. 

Baadhi ya Wakazi wa Njombe  walioshuhudia mazoezi ya  Club wameonesha  kuvutiwa kujituma kwenye  mazoezi hayo  chini ya Mwalimu nguli Bw. Gabriel Mazika, huku wapenzi wa Club hiyo yenye wachezaji mahiri na machachari  wakiwa na matarajio makubwa ya ushindi wa kishindo.