Mahakama ya Rufani Yarejesha Shughuli za Kisiasa za Chadema

Global Publishers
April 15, 2026
0 Comments

Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo itatolewa baadaye Saa 9:00 Alasiri.