MALIASILI YAIBAMIZA VIWANDA 2-1, KAMBA ME NA KE ZAZIDI KUPAA

…………

Na Sixmund Begashe, Njombe 

Timu ya mpira wa Miguu  Wizara ya Maliasili na Utalii umeonesha ubabe usio wakawadia dhidi ya timu ya Wizara ya Viwanda na Biashara maarufu kama Viwanda katika michezo ya Mei Mosi 2026 inayoendekea Mkoani Njombe

Mashabiki wa timu hiyo ya Makiasili waliojitokeza kwa wingi kuishalia timu yao walisikika wakisema kuwa  wameridhishwa na uwezo wa timu na kuwa wanaoendelea kuiombea izidi kushinda kwenye Michuano ijayo. 

Akizungumza mzia mchezo huo, Kocha wa Maliasili Bw. Lusinde Yusuph Nyingi amekiri kuwa wapinzani wao hawakuwa wepesi bali kilichopelekea washinde ni uwezo mkubwa wa wachezaji unaotokana na mazoezi ya hali ya juu. 

Naye Naodha wa Timu ya Viwanda Dkt. Hamed Kijazi ameipongeza timu ya Maliasili kwa ushindi walio upata huku akisema ushindani huo unawapa nafasi ya kujipanda zaidi na michezo ao mingine.

Katika hatua, nyingine timu ya Kamba Maliasili wananawake imeiburaza 2-0  timu ya  Ujenzi huku Maliasili Wanaume Kamba wakishinda 1 dhidi ya Timu ya Wizara ya Fedha.