“NGUVU KAZI SHINDANI NI KETE YA DIRA 2050”- DAVID KAFULI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulila.

****

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulila, amesema makusanyo ya kodi na mikopo pekee hayawezi kutosheleza mahitaji makubwa ya kuleta ustawi kwa Watanzania, hivyo ushirikishwaji wa sekta binafsi ni wa lazima.

Kafulila amefafanua kuwa Serikali inayolazimisha kufanya kila kitu peke yake hujikuta ikishindwa kutoa huduma bora za msingi, hususani katika sekta za elimu na afya, ambazo ndio nguzo za kujenga rasilimali watu.

Kafulila alihitimisha kwa kutoa dira ya kimkakati inayosukuma ajenda ya PPP. Alieleza kuwa iwapo Serikali itatumia mitaji ya sekta binafsi kujenga miundombinu, itaokoa fedha nyingi ambazo sasa zitapelekwa moja kwa moja kugharamia afya na elimu bora kwa jamii maskini isiyoweza kumudu gharama hizo.

“Dunia ya leo tunazungumzia ushindani wa watu, sio vitu. Ushindani wa watu wenye ubora. Hawa watu wenye ubora unawatengeneza je kama hauna bajeti ya kutosha? …Kwa kupitia ubia Serikali inaokoa fedha nyingi itazielekeza kwenye kujenga rasilimali watu… ambayo itaweza kujiunga kwenye klabu ya mataifa tajiri duniani mwaka 2050,” alihitimisha Mkurugenzi.